Monday, July 30, 2018

NIYONZIMA KUTOENDA TENA UTURUKI

Kiungo wa klabu ya soka ya Simbasctanzania #HarunaNiyonzima sasa hatoweza tena kuungana na wenzake nchini #Uturuki lakini pia huenda kiungo huyo fundi akakutana na adhabu kutoka uongozi wa klabu ya soka ya Simba Sc kutokana na kile kinachoaminika kuwa ni utovu wa nidhamu.

Akizungumzia kuhusu hilo Kaimu mwenyekiti wa Simbasctanzania Bw. Abdallah maarufu kwa la "Try Again" alisema, " Haruna Niyonzima baado ni mchezaji wa simba sc na anakiwango kikubwa cha kuisaidia simba sc tulimpa ruhusa maalum  ya mapumziko pamoja na matibabu kwao Rwanda,alitakiwa arudi tarehe 20 ili aweze kuungana na wanzake  na hata passport yake tayari inavisa ya Uturuki lakini  kwa sababu ambazo tumeshindwa kuzifahamu mpaka sasa kwanini Haruna hajajiunga na timu kwaajili ya preseason sisi kama uongozi akirejea tutamwita na tutamhoji kwanini amechelewa tutamsikiliza nini kimemchelewasha  kabla hatujamuadhibu kulingana na taratibu zetu pindi mchezaji anapofanya kosa basi hoja atakazotupa tutashauriana na mwalimu kama ataweza kumpa program maalum ili accompasate yale waliyofanya wenzake lakini kwa sasa hatokwenda tena Uturuki maana siku zimekwisha".

Kwa taarifa hiyo huwenda kiungo huyo akakumbana na adhabu kali ili kuwa fundisho kwa wachezaji wengine endapo sababu zake zitakosa mashiko.

No comments:

Post a Comment