Omary Faraji Nyembo (amezaliwa tar. 12 Septemba, 1987) ni jina la mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka
nchini Tanzania ambaye anajulikana kwa jina la kisanii kama Ommy Dimpoz. Ommy alianza kusikika
kwenye wimbo wa Utamu Iliyotoka 4/12/2012 alioshirikishwa na Dully Sykes,
Lakini alianza kuvuma kwa wimbo wake wa Nai Nai iliyotoka
2/07/2014, aliomshirikisha Ali Kiba, Baadaye Iliyotoka 03/07/2014, Me
and You Iliyotoka 2/07/2014, alioshirikishwa
na Vanessa Mdee, Mama Iliyotoka 13/04/2015, alioshirikishwa na Christian Bella, Hello Baby alioshirikishwa
na Avril kutoka Kenya, Cheche Iliyotoka 23/09/2017, Achia Body Iliyotoka19/12/2015, Tupogo iliyotoka 22/05/2014, Ndagushima Iliyotoka 16/05/2014, Wanjera Iliyotoka 12/03/2015, Kajiandae Iliyotoka 5/05/2016, Aliomshirikisha AliKiba Na Wimbo wake
latest unaojulikana kama Yanje Iliyotoka 1/may/2018 aliomshirikisha
msanii Seyi Shay kutoka nchini Naigeria. Ommy Dimpoz ni msanii mwenye masihara na
maneno mengi ya kuchekesha. Sawa na Rayvanny wa WCB. Ommy ni moja kati ya
wasanii ambao wanajali sana faragha za maisha yao. Awali mwaka 2016 kulikuwa na
gumzo kubwa baada ya Nay wa Mitego kumwimba vibaya Ommy kwenye wimbo wake na
kumshutumu kama shoga. Baadaye Ommy akajibu kwa kuonesha picha ya mwanamke
wake.[2] Ommy ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Pozi kwa Pozi
Entertainment ambayo meneja wake (Mubenga) aliachia ngazi mwaka wa 2016.[3] Tangu wimbo wa Cheche (2017), amekuwa chini ya lebo
ya Rockstar4000 ambayo
iko chini ya Ali Kiba.
Mwaka
2018 umekuwa mbaya kwa msanii Ommy Dimpoz kutokana na ugonjwa wa koo
unaomsumbiua sana na hatimae kupelekwa nchini south Afrika kwa matibabu. Ambapo
alifanyiwa upasuaji na kuruhusiwa hivi karibuni tena amelirudishwa hospital kwa
uangalizi Zaidi baada ya kusikika kwamba hali imezidi kuwa mbaya Zaidi. Ingawa
wengine wamekuwa wakitoa taharifa ya kwamba amepelekwa chumba cha uangalizi
maalumu inayojulikana kama ICU, lakini kwa upande wa mameneja wake wamekanusha
na kusema taharifa hizo ni za uongo mkubwa.


No comments:
Post a Comment