Sunday, August 26, 2018

BARAKA DA PRINCE ATOA DARASA KWA WASANII AMTOLEA MFANO ALIKIBA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Baraka The Prince amewataka wasanii ambao wana vipaji zaidi ya kimoja kuvitumia kwani ni moja ya sehemu ya kupiga mkwanja nje ya maisha ya muziki.

Barakah akiongea na Bongo5, amesema kuwa hata yeye ni mchezaji mzuri wa kikapu na kama akiapata chansi ataenda kucheza huku akimbariki msanii mwenzake Alikiba kwa kujiunga na klabu ya Coastal Union.
Akikazia ishu ya Alikiba kujiunga na Coastal Union, Barakah amesema kuwa hiyo ni hatua nzuri kwake kwani itamsaidia kuongeza fanbase na kipato pia, huku akisema kuwa hata yeye akipata chansi kama hiyo anaweza kucheza Ligi ya Kikapu.
TOA MAONI YAKO HAPA

No comments:

Post a Comment