Msanii wa
muziki Bongo Mbosso amesema si kweli kwamba wimbo wake unaokwenda kwa jina la
Nimekuzoea alimuimbia Diamond Platnumz baada ya kuachwa na mzazi mwenzie, Zari
The Bosslady.
Muimbaji
huyo kutokea WCB katika mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema wimbo huo
ulikutana na tukio hilo na ulikuwepo kwa kipindi kirefu. "Hapana, ni wimbo
ambao ulikutana tu na tukio, ni wimbo wangu ambao nilishawahi kuimba zamani
sana kipindi nipo Yamoto Band," amesema. "Sasa nilipokuja kuingia WCB
ni moja ya nyimbo zangu alikuwa anazipenda sana Bosi (Diamond), akaniambia
inabidi uufanye, sasa kipindi ambacho nautoa ndio ua mwana wa weusi," amesema Mbosso.
Wimbo wa Mbosso, Nimekuzoea ulitoka February 09,
2018 wakati usiku wa February 14, 2018 ambayo ilikuwa ni siku ya Wapendanao
(Valentine Day) ndipo Zari The Bosslady aliposti Ua Jeusi kwenye ukurasa wake
wa Instagram na kueleza ameachana rasmi na @DiamondPlatnumz

No comments:
Post a Comment