Imechukua muda kidogo toka kundi bora la muziki duniani ambalo lilikuwa linaundwa na mapacha wawili #PSQUARE kuvunjika hapo hakuna mmoja kati yao ambaye alijitokeza na kusema sababu hasa za undani za kuvunjika kwa kundi hilo.
Ila moja ya founder wa kundi hilo Peterpsquare amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya sababu za kuvunjika kwa kundi hilo.
Well Peterpsquare amesema sababu kubwa kabisa ya kundi hilo kuvunjika ni kutokana na his twin brother Rudeboypsquare kushindwa kuiheshimu familia yake kwa maana mke wake na watoto pia.
Amepata nafasi ya kuzungumza hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na kituo cha Citizentvkenya.
Kwa upande mwingine msanii huyo ameonekana kwenye picha ya pamoja na msanii anayekimbiza kunako game ya bongofleva Benpol na kuzua maswali kwamba huenda kuna kazi inakuja baina ya wasanii hao wawili.


No comments:
Post a Comment