Monday, July 30, 2018

SAHAU STORY YA WASAFI FM MWAKA 2018, HADI 2019 ASEMA DIAMOND PLATNUMZ

Diamond Platnumz amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ni lini kituo chake cha radio cha Wasafi FM kitaanza kurusha matangazo kama ilivyo kwa kituo chake cha Runinga cha Wasafi TV.

Habari nzuri ni kwamba Diamond amesema Wasafi FM itaanza kurusha matangazo yake mwezi Januari mwakani huku akieleza mipango yake ya kupanua wigo wa matangazo kwa Wasafi TV.
“Nimefungua Tv inaitwa Wasafi TV na inafanya vizuri sana na tupo katika mikakati ya kuhakikisha inapatikana bara zima la Afrika na ulimwenguni kote. Lakini pia mwezi wa kwanza au mwishoni mwa mwaka huu tunafungua pia Wasafi FM itakuwa hewani.“amesema Diamond Platnumz kwenye mahojiano yake na kituo cha radio cha Mayotte la 1ère cha kisiwani Mayotte alipoulizwa na moja ya matu waliopiga simu studio kumuuliza kama anamiliki vituo vya Radio na Runinga.

Wikiendi iliyopita Diamond Platnumz alikuwa Mayotte na alifanya show babkubwa kwenye visiwa hivyo vya Ufaransa. Tazama mahojiano yake na kituo hicho cha radio kwa lugha ya Kifaransa.

No comments:

Post a Comment