Thursday, August 23, 2018

SERENA WILIAMS AONGOZA KWA WACHEZA TENNIS WA KIKE WALIOINGIZA MKWANJA MKUBWA 2018

Serena Williams Amekuwa na Kawaida ya Kuvunja Record nyingi zaidi kwenye upande wa Mpira wa Tennis na kila kukicha anatangazwa kubeba vikombe kwenye ligi tofauti anazoshiriki za mchezo huo.

Hii ni Record nyingine tena ya kutangazwa kuwa mchezaji wa Kike kwa épande wa Tennis anayeongoza kwa kuingiza pesa nyingi zaidi kwa mwaka 2018 kwa mujibu wa Jarida maarufu la Forbes huku akiwapiku mastaa kibao kwenye mchezo huo .
.
@serenawilliams amefanikiwa kuingiza kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 18.1 sawa na takribani Bilioni 41 kwa pesa za Kitanzania, huku akifuatiwa na Caroline Wozniacki ambaye ni mchezaji kutokea Denmark kwa kiasi cha Dola Milioni 13 na Sloane Stephens ambae ni Mmarekani anashikilia nafasi ya tatu kwa kiasi cha Dola Milioni 11

Kiasi hicho kilichokuja kutokana na uwekezaji wa makampuni (endorsements) kinamfanya mshindi huyo mara 23 wa mataji ya Grand Slam kuongoza list hiyo iliyotawaliwa na wachezaji wa tenisi kwa mwaka watatu mfululizo.

No comments:

Post a Comment